Dec
28
2012
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika makazi
ya padri Ambrose Mkenda wa Paroko wa parokia ya kanisa katoliki la
Mpendae Zanzibar kuupa pole uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia
yake kufuatia ajali ya kupigwa risasi hivi karibuni na watu
wasioujulikana.
Tukio hilo la kusikitisha lililofanywa na watu wawili waliopakiana
kwenye Vespa lilitokea langoni mwa Skuli ya Francis Maria iliyopo
Tomondo Wilaya ya Magharibi ambapo ndio makaazi ya Padri Ambrose.
Balozi Seif akiufariji Uongozi huo alisema ni jambo baya na la
kusikitisha lililofanywa na watu hao ambalo limetoa sura mbaya kwa Taifa
na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea kufanya
uchunguzi wa tukio hilo na haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria
watu watakaobainika kufanya uhalifu huo.
Alisema Serikali imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao
ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi
katika hali ya wasi wasi usio wa lazima ndani ya harakati zao za
kimaisha.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi na Familia ya Padre Ambrose
Mkenda Kiongozi kutoka Kanisa la Roman Catholic Father Shayo aliiomba
Serikali kuendelea kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu
iliyotanda mioyoni mwao kutokana na matukio ya uvamizi.
Father Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na
baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima
kwa sababu ya utofauti wa Kidini inawajengea maisha mabovu watoto hao. “
Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine tuelewe
kwamba Taifa halitakuwa na muelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye”.
Alitahadharisha Father Shayo.
Na Othman Khamis Ame
No comments:
Post a Comment