30 Aprili, 2013 - Saa 08:49 GMT
Wasomi nchini
Australia wametaka mpasuaji wa kichina anayetuhumiwa kufanya biashara
haramu ya viungo vya mwili kuvuliwa taji la mtaalamu alilopewa katika
chuo kikuu cha cha Sydney.
Huang Jiefu, aliyesomea taaluma hiyo huko
Sydney, hivi maajuzi aliongezewa muda taji hilo la kuwa Profesa kwa
miaka mitatu inayokuja.Chuo kikuu cha Sydney ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyo na sifa kuu nchini Australia.Mnamo mwaka 2005 Huang Jiefu,alikuwa afisa mkuu wa kwanza wa afya aliyefichua mtindo wa China kutoa viuongo vya mwili kutoka kwa wafungwa.
Na anatazamwa na wengi kama aliyeleta mageuzi katika katika mfumo huo unaoshutumiwa kwa ukubwa.
Kwa waliopanga ombi la kutaka apokonywe taji alilopewa wanaona kwamba anahusika na mfumo huo usio na maadili na amehusika katika hilo kwa kufanya upasuaji wa kutoa ma kubadili viungo hivyo.
Wanadai kuwa yeye na maafisa wa serikali Beijing wametoa malipo ili kusitisha biashara hiyo haramu.
Kw amujibu wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu China huua wafungwa takriban 4000 kila mwaka kwa kutumia sindano yenye sumu ili kutoa viungo hivyo katika miili ya wafungwa hao.
No comments:
Post a Comment