Pamoja na ukweli kwamba filamu za Tanzania zimefika katika hatua nzuri kwa sasa katika nyanja za uandishi, utayarishaji, usambazaji na mauzo ukilinganisha na miaka kama mitano iliyopita, bado kuna kasoro za hapa na pale.
Kasoro ni nyingi kulingana na uchanga wa tasnia hiyo ukilinganisha na filamu za kimataifa lakini ni suala linaloweza kuvumilika kutokana na ukweli huo.
Lakini kuna baadhi ya wadau wamekuja na sababu kadhaa za utani ambazo zinatambulisha filamu za Bongo nazo ni:
1. Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke barabara.
2. Matajiri majumba yao yana askari badala ya electric fence & gates.
3. Trailer inachukua dakika 40.
4. Part2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part1 ilikuwaje.
5. Mademu wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.
6. Wakifika hotelini imezoeleka ni juice inaagizwa au wine isiyofunguliwa.
7. Nusu saa mtu anatembea,anafanya mazoezi, anakimbizwa ananunua vitu.
8. Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.
9. Mtu yupo village, life gumu ana wave kichwani.
10. Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.
11. Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara.
12. Tajiri anakuja kumpenda maskini.
No comments:
Post a Comment