Wednesday, June 5, 2013

MAMBO 12 YANAYOIFANYA BONGO MOVIE IDHARAULIKE


Pamoja na ukweli kwamba filamu za Tanzania zimefika katika hatua nzuri kwa sasa katika nyanja za uandishi, utayarishaji, usambazaji na mauzo ukilinganisha na miaka kama mitano iliyopita, bado kuna kasoro za hapa na pale. 


Kasoro ni nyingi kulingana na uchanga wa tasnia hiyo ukilinganisha na filamu za kimataifa lakini ni suala linaloweza kuvumilika kutokana na ukweli huo. 

Lakini kuna baadhi ya wadau wamekuja na sababu kadhaa za utani ambazo zinatambulisha filamu za Bongo nazo ni:

1. Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke barabara.

2. Matajiri majumba yao yana askari badala ya electric fence & gates.


3. Trailer inachukua dakika 40.


4. Part2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part1 ilikuwaje.


5. Mademu wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.


6. Wakifika hotelini imezoeleka ni juice inaagizwa au wine isiyofunguliwa.


7. Nusu saa mtu anatembea,anafanya mazoezi, anakimbizwa ananunua vitu.

8. Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.


9. Mtu yupo village, life gumu ana wave kichwani.


10. Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.


11. Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara.


12. Tajiri anakuja kumpenda maskini.

Saturday, June 1, 2013

ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA JINSIA MOJA.....UKINASWA IMEKULA KWAKO ( MIAKA 30 JELA )



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. 


Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

KIBAKA ACHOMWA MOTO HUKO MBAGALA BAADA YA KUIBA BEGI NA SIMU...


Jamaa  akimmalizia mtuhumiwa kwa  tofali...
 Kibaka  mmoja  amejikuta  akiyaaga  maisha ya  uraiani  baada ya   kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali....

Tukio hili limetokea maeneo ya mbagala charambe mida ya saa sita mchana baada ya kibaka huyu kuingia  ndani ya nyumba ya mtu na kuiba begi...

Taarifa zinaeleza kwamba, raia mwema ambaye ni mkazi wa nyumba hiyo alisahau kufunga mlango  na  kwenda kwa jirani...Alipotoka tu, Kibaka huyo alizama   ndani na kuchukua begi la nguo taratiiibu kama lake! 

Hakuridhika na begi,  alivyotazama pembeni aliona kuna  simu .Bila  kupoteza muda, kibaka huyo aliihifadhi mfukoni ..

Balaa  liliazanza wakati anajiandaa  kutoka...Alipofika  mlangoni, kibaka huyo alikutana na mwenye nyumba uso kwa uso.....!!! 

SINEMA ILIANZIA HAPO!!!!! Watu mwiziii... mwiziiii mwiziiiiiiiiiii....!!!!! 

Kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu, jamaa huyo alibahatika kujisweka ndani  jumba bovu lililoko uchochoroni na kuinusuru roho yake....

Raia wenye hasira kali hawakumuona wakapita, Kufika mbele kidogo walikata tamaa. Wakati wanarudi nyumbani kwao mara ghafla  jamaa  akakurupuka na  kuchomoka kwenye dirisha la lile jengo bovu alikokuwa amejificha....
 
Harakati zikaanza upyaaaaaa!!!!! YAAAANI...!! jambazi hakuchukua raundi akatiwa mikononi... 

MPENDWA msomaji,   mambo yalienda kama tunavyoona hapo pichani.
Moto unawaka!
 Tairi limeletwa
Mwizi  amevishwa tairi na kutiwa moto!

masaimbofu

Chuck Hagel accuses China of 'cyber intrusions' on US

June 1, 2013 US Defense Secretary Chuck Hagel has accused China of waging cyber espionage against the United States, stepping up pressure on Beijing over the issue ahead of a key bilateral summit.
Chuck Hagel: Chuck Hagel accuses China of 'cyber intrusions' on US
Chuck Hagel accuses China of 'cyber intrusions' on US  Photo: AP
Speaking at a Singapore security forum attended by senior Chinese military officials, the Pentagon chief pointedly blamed the Chinese government and armed forces for repeated intrusions into sensitive US information systems.
"The United States has expressed our concerns about the growing threat of cyber intrusions, some of which appear to be tied to the Chinese government and military," he told an annual conference known as the Shangri-La Dialogue.
Hagel pressed Beijing to adhere to "international norms of responsible behaviour in cyberspace", while acknowledging that the establishment of a joint cyber security working group was a positive step in fostering US-China dialogue on such issues.
The Singapore forum came ahead of the June 7-8 meeting between US President Barack Obama and his Chinese counterpart Xi Jinping in California, the two leaders' first meeting since Xi took office in March.
China's delegation to the Singapore meeting was led by Lieutenant General Qi Jianguo, a deputy chief of the general staff of the People's Liberation Army.

Thursday, May 23, 2013

DAKTARI AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI HUKO MOROGORO


 


DAKTARI wa meno Anorld Rimo (umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya Sabasaba manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda. 

Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika 

nyumba hiyo ya kulala wageni.

Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo. 

Ameeleza kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo  na kufanya fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi. 

Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi.

Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi.

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA MAMILIONI JIJINI DAR LEO SAA TANO ASUBUHI

 Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) ,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.
 
Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.
 
Mmoja wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali).

Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.

MKURUGENZI WA MASHITAKA NCHINI ATAKA LWAKATARE ASHITAKIWE KWA UGAIDI TENA



MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha ombi katika Mahakama ya Rufaa nchini, akiomba itengue uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wa kumfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Dk. Feleshi aliwasilisha ombi hilo juzi kwa njia ya maandishi, ambapo katika maombi yake anaiomba mahakama hiyo iitishe mwenendo wa shauri lililotolewa uamuzi huo na Jaji wa Mahakama Kuu, Lawrence Kaduri Mei 8, mwaka huu na kuupitia upya na ifute uamuzi huo kwa kuwa una makosa kisheria.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Dk. Feleshi anadai Mahakama Kuu haikuombwa kumfutia mashitaka Lwakatare kama Jaji Kaduri alivyotoa uamuzi huo, bali aliiomba mahakama iitishe majalada ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na 20 mwaka huu.

“Kwa kuwa Ofisi ya DPP ipo kwa ajili ya kusimamia utawala wa sheria, haijaridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliomfutia mashitaka matatu Lwakatare, hivyo tunaiomba mahakama hii iitishe mwenendo wa kesi ulioamuliwa, kwani tunaamini kisheria jaji alikosea kutoa uamuzi ule, kwani Lwakatare hakuwa ameomba afutiwe mashitaka yanayomkabili,” alidai Dk. Feleshi.

Hata hivyo hadi jana mchana uongozi wa Mahakama ya Rufaa ulikuwa bado haujapanga majaji wa kusikiliza ombi hilo.