HISTORIA YA MASWAHABA
HISTORIA FUPI YA SAYYIDNIA OMAR (R.A.)
‘Umar bin Al-Khattwaab
(Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa kila linapotajwa jina la Abu Bakr
(Radhiya Allaahu ‘anhu) akisema; "Bwana wetu aliyemkomboa Bwana wetu".
Akimkusudia Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wanasema
wanavyuoni kuwa; Unapomsikia ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akimwita mtu
'Bwana wetu', basi tambua ya kuwa huyo ni mtu adhimu. Imeandikwa katika
Siyar al-A’alaam an- Nubalaa kuwa Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye
asili yake ni Mhabeshi (mu- Ethiopia), alikuwa mweusi sana, mwembamba,
mrefu na mwenye nywele ndefu. Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa
mtumwa wa kabila la Bani Jumhi, na maisha yake yalikuwa kama mtumwa
yeyote wa kawaida pale Makkah, hakuwa na uwezo wala uhuru wowote
isipokuwa
kuwatumikia mabwana zake watu wa kabila la Al-Jumhi.
Baadaye alimilikiwa na Umayyah bin Khalaf peke yake ambaye pia anatokana
na kabila hilo la Al- Jumhiy, na mama yake Bilaal na jina lake lilikuwa
Hamaamah, naye pia alikuwa mtumwa wa kabila hilo la Al-Jumhi. Mara
baada ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuanza kuwalingania
watu katika dini ya Kiislam kwa jahari, Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu)
akawa anasikia habari za dini hii mpya na habari za Mtume huyu mpya
(Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na habari hizo zilikuwa
zikimfurahisha sana kila anapozisikia hasa kutoka kwa Abu Bakr
Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa kila anapopata fursa
akimwendea Bilaal na watu wengine pia na kuwahadithia juu ya dini hii.
Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasilimu mikononi mwa Abu Bakr
Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akifanya kazi kubwa sana
tokea siku ya mwanzo katika kuwalingania watu katika dini hii tukufu.
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akiwalingania watu waliokuwa
huru na akafanikiwa
kuwasilimisha watu watukufu wakiwemo watano
katika wale kumi waliobashiriwa Pepo nao ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan,
Az-Zubayr bin ‘Awaam, ‘Abdur- Rahmaan bin ‘Awf, Sa’ad bin Abi Waqaas na
Twalha bin ‘UbayduLlaah (Radhiya Allaahu ‘anhu) na wengi wengineo, na
alikuwa pia akiwalingania watu wasiokuwa huru kama vile Bilaal (Radhiya
Allaahu ‘anhu) aliyekuwa rafiki yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)
tokea hata kabla ya Uislam, na wengineo pia. Bilaal (Radhiya Allaahu
‘anhu) alifuatana na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) mpaka kwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na kuzitamka shahada
mbili mbele yake, na kwa ajili hiyo akawa miongoni mwa watu wa mwanzo
kuingia katika dini hii tukufu. Ahadun Ahad Uislam ulipoanza kuenea
katika mji wa Makkah, na baadhi ya Ma-Quraysh kutambua kuwa watumwa wao
walikuwa wakiingia katika dini hii mpya kwa siri tena kwa wingi,
wakaanza kuwatesa kwa kuwaonjesha kila aina ya adhabu. Miongoni mwa
Waislam wa mwanzo waliokuwa watumwa na wakapata adhabu kubwa kutoka kwa
washirikina wa Makkah, ni Sumayyah, mama yake ‘Ammaar aliyekuwa mke wa
Yaasir (Radhiya Llaahu ‘anhum) waliokuwa na asili ya Ki-Yemen. Walikuwa
wakiadhibishwa sana, na kila Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam)
anapopita nje ya nyumba yao alikuwa akiwaambia; "Kuweni na subira enyi
watu wa nyumba ya Yaasir, kwani hakika waadi wenu ni Pepo". Sumayyah
(Radhiya Allaahu ‘anhu) alifariki akiwa anateswa na akapata bahati ya
kuwa
Shahid wa mwanzo katika dini ya Kiislam. Bilaal (Radhiya
Allaahu ‘anhu) naye alipata sehemu kubwa ya adhabu, kwani bwana wake
Umayyah bin Khalaf aliyekuwa mtu khabithi sana, alikuwa akimtoa nje
wakati wa jua kali linalounguza mwili na kumvua nguo zake kisha anamlaza
juu ya mchanga wa jangwani unaounguza na kumwekea jiwe kubwa sana juu
ya kifua chake huku akimwambia; "Utabaki hivyo hivyo mpaka ufe isipokuwa
kama utamkanusha Muhammad na kumtukana kisha urudi tena kuiabudu miungu
yako Lata na Uzza". Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akimjibu kwa
kusema; "Ahadun Ahad".(Mmoja tu, mmoja tu) Bilaal (Radhiya Allaahu
‘anhu) aliwahi kuulizwa; "Kwa nini ulikuwa ukiendelea kusema hivyo
"Ahadun Ahad". (Mmoja tu, mmoja tu), na hali unajua kuwa maneno hayo
yanawaghadhibisha na kwa ajili hiyo wao wataendelea
kukuadhibu?"
Akajibu; "WaLlaahi kama ningekuwa nalijuwa neno jingine linaloweza
kuwakasirisha zaidi kuliko hilo, basi ningelilitamka". Hakika neno;
"Ahadun ahad", lilikuwa likimkera sana Umayyah na kila anapolisikia
alikuwa ghadhabu zinampanda na akawa anampiga Bilaal (Radhiya Allaahu
‘anhu) kama mwendawazimu. Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akawa
anaendelea
kuadhibishwa na yeye alikuwa akiendelea kustahamili huku
akiendelea kulitamka neno lake hilo 'Ahadun ahad', mpaka Umayyah
mwenyewe
akashindwa, kwani kila siku baada ya kumtesa wakati wa
mchana, alikuwa akimfunga kamba shingoni na kuwakabidhi watoto wadogo na
wendawazimu
waliokuwa
wakimburura Bilaal (Radhiya Allaahu
‘anhu) na kuzunguka naye mjini Makkah, huku wakimzomea na kumpiga, na
yeye alikuwa akiendelea kusema'
No comments:
Post a Comment