Wednesday, May 15, 2013

Kukosekana kwa viwango vya elimu kikanda kunazuia ukuaji wa biashara katika Afrika Mashariki

Kushindwa kutekeleza mfumo wa elimu ya kawaida yenye sifa zilizowekwa katika kiwango kilichokubalika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kumezuia mtiririko wa fursa za rasilimali watu na biashara, wadau wasema.
  • Mhandisi wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Kenya akisimamia mifumo katika chumba cha kudhibiti umeme unaozalishwa kutokana na maji ya bwawa. Kwa kuwa na viwango vya elimu vyenye uwiano, wahandisi wangeweza kufanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zina uhitaji mkubwa. [Tony Karumba/AFP] Mhandisi wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Kenya akisimamia mifumo katika chumba cha kudhibiti umeme unaozalishwa kutokana na maji ya bwawa. Kwa kuwa na viwango vya elimu vyenye uwiano, wahandisi wangeweza kufanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zina uhitaji mkubwa. [Tony Karumba/AFP]
"Kila nchi ina viwango tofauti katika kuajiri wafanyakazi kwa sababu ya kutofautiana kwa mfumo wa elimu," alisema Patrick Obath, mjumbe wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, asasi mama ambayo inawezesha ushiriki wa sekta binafsi katika mchakato wa kujumuisha EAC.
"Jambo hili linazuia uwezo wa kuwepo, mfano, raia wa Uganda kufikiriwa katika kazi nchini Kenya au Tanzania na kinyume chake," aliiambia Sabahi. "Hili linazuia utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja."
EAC, makao makuu yako Arusha, Tanzania, ni asasi baina ya serikali ambayo inadhamiria kupanua ujumuishaji wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni baina ya Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Obath alisema kushindwa kurahisisha fursa za ajira nje ya mipaka kumefanya mchakato wa ujumuishaji wa EAC na ushindani wa kikanda kwa ujumla kwenda taratibu.
Uwianishaji wa mifumo ya elimu na mitaala ya mafunzo ilianza 1998, wakati ofisi ya kudumu ya EAC ilipopewa dhamana ya kufanya utafiti wa ulinganifu wa kikanda kusawazisha falsafa za elimu, maudhui ya mitaala, miundo ya elimu, sera na mfumo wa kisheria.
Lakini kutoka hapo, mchakato ulizuiwa. Mwaka 2003, kamati ya ushauri ya EAC kuhusu elimu, utafiti na mafunzo iligundua kuwa mchakato wa kuwa na wataalamu wa elimu wa kikanda kuunganisha mitaala ulikuwa unachukua muda mrefu. Kisha, mwaka 2008, uelekezi kuhusu elimu ulisimamishwa kwa sababu ya kukosa fedha za kutosha.
Obath anasema mchakato huo unaendelea kuzuiwa na hali ya kuwa na mashaka ya wanachama wa EAC na kukosa fedha na utashi wa kisiasa.

Uwiano wa elimu 'siri ya kukua'

Vimal Shah, ofisa mtendaji mkuu wa Bidco Oil Refineries Limited, wazalishaji wa bidhaa za majumbani wanaoongoza Afrika Mashariki, alisema imekuwa vigumu kuajiri wafanyakazi katika mtambo wa kampuni kwa sababu ya viwango tofauti.
"Hatuwezi kuwa na wahandisi kutoka Uganda wakifanya kazi katika mtambo wetu nchini Kenya. Kwa sababu ya tofauti ya [taratibu za] mafunzo, hawawezi kupata leseni kufanyia majaribio nchini Kenya," alisema. "[Huu] ni udhia na gharama kubwa kwa biashara, tatizo ambalo linaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuwianisha viwango vya uteuzi."
Peter Mathuki, mjumbe wa Baza la Wawakilishi la Afrika Mashariki, alilalamikia maendeleo ya polepole katika uwianishaji wa viwango vya elimu.
"Elimu na sifa ni msingi wa kuingiliana katika kanda, na bila kuwa na viwango vinavyofanana ni vigumu kwa wananchi wetu kwenda kufanya kazi nje ya mipaka yetu kama ilivyoridhiwa katika itifaki ya soko huria," Mathuki aliiambia Sabahi. "Ninajua ni changamoto kwa biashara ambazo zinavuka nje ya mipaka."
Japokuwa kulikuwa na utayari wa kisiasa kutoka kwa viongozi wa EAC, urasimu ndani ya wizara za elimu za kila nchi umesababisha kukaidi kuhusisha timu zao za ufundi kubadilisha sera za elimu ili kukidhi katika kanda, alisema.
Ukaidi huu wa teknokrasia unachapuzwa na woga kwamba baadhi ya nchi zina ushari zaidi na kwamba kama kungekuwa na mfumo wa elimu unayofanana, wananchi wake wangekuwa na uwezo wa kukamata fursa zote za juu za ajira katika kanda na kuwa hasara kwa wengine wanaobaki," alisema. "Huu ni uvumi, kwa sababu mfumo huohuo utatuwezesha kujenga umoja na kuwa na uwezo wa kushindana. Hii ni siri ya kukua kwetu."

Baraza la Chuo Kikuu latafuta mamlaka ya kufanya mabadiliko

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Egerton James Tuitoek alisema Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariiki (IUCEA), ambalo liliundwa chini ya EAC mwaka 2009 kama njia ya kuratibu na kushirikiana miongoni mwa vyuo vikuu na kuimarisha viwango vya elimu vinavyolinganishwa kimataifa huko Afrika Mashariki, limekabiliwa na kutokuwa na fedha za kutosha kugharimia programu zake.
"Hadi sasa, tupo katika mchakato wa kulinganisha muhtasari, upatikanaji wa elimu na viwango vya ufundishaji vinazingatiwa," Tuitoek aliiambia Sabahi. "Tumeimarisha pia sheria zote kutoka kwa nchi wadau kuhusiana na elimu na tumewasilisha marekebisho kwa kila nchi ili kuwezesha usawazishaji."
Tuitoek, ambaye alikuwa mjumbe wa baraza hilo, alisema biashara sio tu pekee zinazokabiliwa na changamoto kutokana na kushindwa kuwa na mfumo wa elimu inayofanana kwani taasisi za mafunzo zinakabiliana na masuala hayohayo.
"Kwa mfano, vyuo vikuu vimeweka kampasi katika nchi nyingine zinalazimishwa kuajiri makamu mkuu wa chuo tofauti, na kuanzisha muhtasari tofauti wa kufundishia kulingana na viwango vya nchi mwenyeji, kitu ambacho kinafanya uwekezaji katika sekta hii kuwa mgumu na wa gharama kubwa," alisema.
IUCEA iliwasilisha idadi kadhaa ya sheria kwenye baraza la kutunga sheria la EAC kulazimisha wanachama kurekebisha mifumo ya elimu ili iendane na itifaki ya soko la pamoja.
Tuitoek alisema kwa IUCEA kuweza kuendelea kwa ufanisi, inapaswa kuwezeshwa kupata utambulisho rasmi katika vyuo vikuu vyote katika kanda