Wananchi waliotaka Zanzibar huru kitaifa na kimataifa ikifuatiwa na muungano wa mkataba kati yake na Tanganyika ni 57.
Na kwaupande wa wananchi waliotaka mfumo huu uliopo wa muungano uendelee kama ulivo kati ya Zanzibar na Tanganyika ni 57.
Saturday, December 8, 2012
Dk Shein akutana na watendaji wizara ya habari
WIZARA ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imeeleza kuwa itahakikisha inaingia katika mfumo wa utangazaji wa Dijitali kwani maendeleo katika ujenzi wa miundombinu yake yanatia moyo na vifaa vyote vinatarajiwa kufika na kufungwa kabla ya Disemba 31 mwaka huu.
Maelezo hayo yametolewa leo na uongozi wa Wizara hiyo, wakati wa mkutano kati ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa Malengo Makuu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha Aprili- Juni 2011-2012 na Julai- Septemba 2012-2013.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki kikamilifu.
Akisoma taarifa ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk alisema kuwa mbali ya juhudi hizo Wizara yake inampango wa kuanza kuitumia studio ya kurekodia filamu na muziki iliyopo Rahaleo sanjari na kurejesha matangazo ya Redio ya masafa ya kati kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurushia matangazo hayo huko Bungi.
Alieleza namna Wizara hiyo ilivyopania kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi na kuunda upya Kamisheni ya Utalii kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya na kuanza kazi ya kuzindua dhana ya Utalii kwa wote katika ngazi zote.
Sambamba na hayo, Wizara hiyo ilieleza mikakati yake iliyoiweka katika kuziimarisha sekta zake kuu nne ambazo ni Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na kueleza mafanikio iliyoyapata pamoja na kuzifanyia kazi changamoto ziliopo.
Akiyataja miongoni mwa mafanikio yaliopatikana katika sekta ya habari Waziri Mbarouk alisema ni pamoja na kufanya vizuri katika majaribio ya utangazaji kwa masaa 24 pamoja na kuunganisha uongozi wa radio na TV na kuwasilisha rasimu ya sheria ya Shirika.
Alisema kuwa katika suala la ujenzi wa mnara wa kurushia matangazo Bungi, utekelezaji wake unakwenda vizuri na wakati wowote majaribio ya matangazo yake yatafanywa.
Kwa upande wa Shirika la Magazeti ya Serikali, limekuwa likitekeleza majukumu yake vizuri na tayari lemeanza uchapishaji wa gazeti jengine jipya la Utamaduni na Michezo.
Uongozi huo ulieleza kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika uendelezaji wa gazeti hilo jipya na limepokelewa vizuri hasa kwa upande wa Unguja na Pemba kutokana na taarifa zake.
Ukieleza kuhusu mafanikio yaliopatikana kwenye gazeti mama la Zanzibar Leo, uongozi huo ulieleza kuwa mauzo yake yanatia moyo sana na limekuwa likionesha mafanikio makubwa katika mauzo ikilinganisha na ilivyokuwa hapo siku za nyuma.
Kwa upande wa sekta ya utalii, uongozi huo ulieleza kuwa juhudi zinachukuliwa katika kuimarisha sekta hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuimarisha uchumi nchini.
Tume ya Utangazaji kwa maelezo ya Wizara hiyo nayo hivi sasa inaenda vizuri baada ya kupata ufumbuzi wa kuwa na Bodi yake huku ikieleza mikakati iliyoweka katika kukiimarisha Chuo chake cha Habari ili kiweze kufikia malengo iliyojiwekea.
Kwa upande wa sekta ya utamaduni na michezo, uongozi huo ulieleza juhudi na mikakati iliyojiwekea katika sekta hiyo hukuikieleza kusikitishwa kwake na kulikotokana na timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kukosa kutimiza kiu ya Rais Dk. Shein ya kuja na kombe la Challenge hapa Zanzibar mwaka huu, na kueleza mafanikio ya sekta ya michezo.
Pamoja na hayo, Wizara hiyo ilieleza changamoto kubwa iliyoipata kutokana na kuporomoka kwa jengo la Beit al Ajaib, ambalo ni ngome ya historia ya Zanzibar na kusisitiza kuwa jitihada inafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mji Mkongwe ya kuondoa kifusi na kuweka miega ili kunusuru hali kabla kuanza matengenezo.
Nae, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipongeza juhudi za Wizara hiyo na kusisitiza haja ya kuendeleza juhudi katika kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara hiyo katika sekta zake.
Kwa upande wa Sekta ya Utalii, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kwa makusudi kuongeza nguvu katika kuutangaza utalii wake kwa kutambua umuhimu na thamani yake katika kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi wan chi.
Alisema kuwa jitihada kubwa zitaendelea kuchukuliwa katika kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii. Sambamba na hayo, alilitaka Shirika la Magazeti ya Serikali kuendelea kujiimarisha zaidi kwani tayari limeanza kuleta matumaini makubwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)