Al-Shabaab wanajaribu kujikusanya huko mkoa wa Hiran wa Somalia baada
ya kukabiliwa na mfululizo wa kushindwa na kupoteza miji ya kimkakati
mmoja baada ya mwengine katika miezi ya hivi karibuni, maafisa wa
usalama wa Somalia wasema.
Ahmed Abdullahi, afisa wa usalama katika mkoa wa Hiran, alisema kuwa
alipokea habari ya harakati ya baadhi ya viongozi wakuu wa al-Shabaab
wanatoroka kutoka maeneo yaliyokombolewa na kuelekea Bulo Burde.
"Kwa mujibu wa kile ambacho tumeambiwa na wakaazi wa Bulo Burde
baadhi ya viongozi wa al-Shabaab kama vile Yusuf Sheikh Isse, amabaye ni
dhamana wa mkoa wa Shabelle ya Kati, na viongozi wengine wamekuwa
wakija mji huu," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Tangu vikosi vya washirika vilipoukamata mji wa Jowhar, makamanda wa
vita wa kikundi hicho wamekuwa wakiondoka kutoka maeneo ya Shabelle ya
Kati na kuelekea Hiran ya mashariki," alisema na kuongeza kuwa vikosi
vya Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM)
vinajitayarisha kuelekea Bulo Burde.
"Jeshi la Taifa la Somalia, kwa msaada wa vikosi vya AMISOM, vimekuwa
katika tahadhari na viko tayari kuikomboa miji michache iliyobakia
katika makucha ya al-Shabaab, ikiwemo Bulo Burde," alisema.
Bulo Burde, ambao uko kilomita 240 kaskazini ya Mogadishu na kilomita 40 kusini mashariki ya
Beledweyne, inachukuliwa kuwa ni ngome ya mwisho imara ya al-Shabaab huko Hiran.
Kwa mujibu wa wakaazi, mamia ya wapiganaji wa al-Shabaab wamejificha
mjini humo, wakijitayarisha kuukinga baada ya kupoteza udhibiti wa miji
mingi ya maeneo ya kusini na kati ya nchi.
Kikundi hicho cha wanamgambo kilitangaza wiki iliyopita kuwa kimeunda kikosi kimoja kipya kinachojulikana "
Kikosi cha Abu Yahya al-Libi", kinachoitwa hivyo kwa jina la kiongozi wa al-Qaida ambaye iliripotiwa kuwa aliuliwa mapema mwaka huu huko Pakistani.
Tarehe 17 Disemba, al-Shabaab iliwaonesha wanachama wa kikosi hicho
kipya katika shughuli iliyofanyika huko Bulo Burde kama juhudi za
kuwapanga upya wapiganaji wake walioshindwa, kwa mujibu wa taarifa za
habari.
Hata hivyo, jaribio la al-Shabaab kujikusanya upya linakabiliwa na vikwazo vingi kutokana na
mizozo ya ndani inayoendelea baina ya uongozi wa al-Shabaab pamoja na matatizo ya kifedha ya kikundi hicho, wachambuzi wa masuala ya usalama wasema.
"Al-Shabaab imepoteza maeneo ya kimkakati ambayo yalikuwa yakileta mapato kama vile
Mogadishu na
Kismayu,
kwa hivyo haitaweza kupata fedha za kutosha kujipanga yenyewe na
kugharamia operesheni zake za kijeshi," alisema Mohamed Ali Mohamed,
kepteni mstaafu wa Idara Usalama wa Taifa la Somalia.
Al-Shabaab haitaweza kulinda Bulo Burde, Mohamed alisema. Kinyume
chake, wapiganaji watarudi nyuma na kuelekea misituni baina ya mikoa ya
Shabelle ya Kati na Hiran kwa ajili ya kujikinga, alisema.
"Kama ambavyo tulivyoona katika miezi iliyopita, wapiganaji wa
al-Shabaab wamekuwa wakirejea nyuma kutoka miji yote bila ya ushindani
mara tu vikosi vya washirika vinapokaribia," aliiambia Sabahi.
"Kujitoa kwa Al-Shabaab kutoka miji ya kimkakati kuelekea maeneo ya
vijijini hakumaanishi kuwa wamechagua kutojihusisha na vita ili kuepuka
kupata hasara kubwa," alisema. Maana yake ni kwamba kikundi hakiwezi
kuhimili mashambulizi na kuyakinga maeneo yaliyo katika udhibiti wao,
kwa hivyo wanachama wake hukimbilia maeneo ya vijijini kwa kujilinda."
Al-Shabaab inawalazimisha watoto kubeba silaha
Wakaazi wa eneo la Bulo Burde walisema kwamba al-Shabaab imewateka
nyara watoto na kuwalazimisha kubeba silaha katika juhudi ya kukinga
mashambulizi kutoka Jeshi la taifa la Somalia na majeshi ya AMISOM.
"Al-Shabaab imewakamata watoto wasiopungua 150 kutoka shule na
madrasa ya Qur'an ambao wametekwa kutoka kote nchini na vijiji vidogo
vinavyoizunguka Bulo Burde," mkaazi Abdinur Dahir mwenye umri wa miaka
46, aliiambia Sabahi.
"Viongozi wa al-Shabaab akiwemo Sheikh Yusuf Ali Ugas, afisa wa
kikundi hicho katika mkoa wa Hiran region, pamoja na viongozi wengine
sasa wapo mjini," alisema. "Wanawataka walimu katika shule za Qur'an na
shule za kawaida kusitisha masomo yao na kuwapeleka wanafunzi wao kwenye
kambi za mafunzo ili waweze kujifunza jinsi ya kutumia silaha na
kujiunga na kikundi hicho katika vita vyake vya jihadi, kama
wanavyodai."
Nasra Abdi, mwenye umri wa miaka 42, anayeuza maziwa safi katika soko
la mji, alisema aliwaona wanachama wa al-Shabaab mitaani, wakiwataka
wakaazi kujiunga na kikundi hicho ili kuulinda mji dhidi ya shambulio
linalotarajiwa kutoka vikosi vya Somalia na washirika.
"Kikundi hiki ni adui wa watu wa Somalia kwa sababu ya vitendo vyao
dhidi ya watu wasio na hatia, hasa vijana ambao wanalazimishwa kubeba
silaha na kupigana kwa ajili hao," alisema.