Thursday, May 23, 2013

DAKTARI AJINYONGA NA KUFA NDANI YA GESTI HUKO MOROGORO


 


DAKTARI wa meno Anorld Rimo (umri wa miaka kati ya 30 hadi 40) wa hospitali ya Sabasaba manispaa ya Morogoro, amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda. 

Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika 

nyumba hiyo ya kulala wageni.

Alisema Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo katika chumba namba 2, na kukutwa amejinyongea dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo. 

Ameeleza kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo  na kufanya fujo na kuonesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi. 

Kamanda huyo alisema marahemu alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi.

Chanzo cha kujinyonga hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi.

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA MAMILIONI JIJINI DAR LEO SAA TANO ASUBUHI

 Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) ,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.
 
Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.
 
Mmoja wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali).

Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.

MKURUGENZI WA MASHITAKA NCHINI ATAKA LWAKATARE ASHITAKIWE KWA UGAIDI TENA



MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha ombi katika Mahakama ya Rufaa nchini, akiomba itengue uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wa kumfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Dk. Feleshi aliwasilisha ombi hilo juzi kwa njia ya maandishi, ambapo katika maombi yake anaiomba mahakama hiyo iitishe mwenendo wa shauri lililotolewa uamuzi huo na Jaji wa Mahakama Kuu, Lawrence Kaduri Mei 8, mwaka huu na kuupitia upya na ifute uamuzi huo kwa kuwa una makosa kisheria.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Dk. Feleshi anadai Mahakama Kuu haikuombwa kumfutia mashitaka Lwakatare kama Jaji Kaduri alivyotoa uamuzi huo, bali aliiomba mahakama iitishe majalada ya kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na 20 mwaka huu.

“Kwa kuwa Ofisi ya DPP ipo kwa ajili ya kusimamia utawala wa sheria, haijaridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliomfutia mashitaka matatu Lwakatare, hivyo tunaiomba mahakama hii iitishe mwenendo wa kesi ulioamuliwa, kwani tunaamini kisheria jaji alikosea kutoa uamuzi ule, kwani Lwakatare hakuwa ameomba afutiwe mashitaka yanayomkabili,” alidai Dk. Feleshi.

Hata hivyo hadi jana mchana uongozi wa Mahakama ya Rufaa ulikuwa bado haujapanga majaji wa kusikiliza ombi hilo.