Friday, November 30, 2012

NEW CONSTITUTION


Wa Mkataba na Muundo wa sasa waumana Z’bar

Katuni ya Katiba
Maoni asubuhi 29 Nov. 2012  FUONI:  Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 54; na waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ili kuipa hadhi Zanzibar na Rais wake ni 74.
Maoni 29 Nov. 2012 jioni KWARARA:  Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 54; na waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ya kuirejeshea Zanzibar nafasi yake kama mshiriki sawa ndani ya Muungano ni 71.

KIMATAIFA



Misri yapitisha rasimu ya katiba


MURSE
Bunge la Misri leo limepitisha mswada wa rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura na wananchi ili kuwa katiba kamili. Mwenyekiti wa bunge hilo Hossam el-Ghiriani ametangaza taarifa hizo mapema hii leo.
Bunge hilo linalotawaliwa na Chama cha Udugu wa Kiislamu ambalo linapingwa na Wakristo na Waliberali limepitisha vifungu 234 vya rasimu hiyo. Mswada huo utapelekwa kwa Rais Mohammed Mursi kwa ajili ya kutiwa saini na kisha kupigiwa kura wiki mbili zijazo. Upande wa upinzani nchini Misri umemtuhumu Rais Mursi na washirika wake kuwa wamepitia juu juu vifungu hivyo kwa lengo la kuupitisha muswada huo haraka ili upigiwe kura.
Kufuatia hatua hiyo, maandamano makubwa yamezuka yakipinga muswada huo. Katiba itakayopitishwa itachukua nafasi ya ile iliyoondolewa baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa taifa hilo Hosni Mubarak.

WAASI WA M23 BADO WAPO GOMA


Waasi wa M23 bado wapo Goma

Waasi wa M23 katika mji wa Goma, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi wa M23 katika mji wa Goma, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa kutoka ndani ya maeneo ya mji wa Goma na Sake zinaonesha kwamba bado waasi wa kundi la M23 la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamo kwenye miji hiyo na wamefanya machache kuthibitisha kuondoka.
Umoja wa Mataifa umesema bado hakuna dalili za kuondoka kwa waasi kwenye mji wa Goma, zoezi ambalo ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa kumaliza mgogoro nchini humo. Naibu mMsemaji wa Umoja huo, Eduardo del Buey, amesema kuwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) vitaanza kuwaangalia waasi wa M23 waliouchukua mji wa Goma na sehemu kubwa ya jimbo la Kivu ya kaskazinilenye utajiri wa madini, kwa kutumia ndege zisizoendeshwa na rubani.
Taarifa zinasema kuwa kumekuwepo na misafara ya vikundi vidogovidogo vya M23 kuingia na kutoka katika eneo hilo lakini umoja wa mataifa hauna uhakika kama waasi hao wamepungua mjni Goma. Waasi wa M23 wamesema kuwa wataukabidhi mji huo kwa serikali hii leo au kesho.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle aliyetembelea eneo la Sake, anathibitisha kwamba bado wapiganaji wa M23 wanaendelea kushikilia ngome zao kwenye milima na viunga vya Sake, huku pia wakijihusisha na uporaji katika maeneo wanayoyakalia.

Sikiliza ripoti ya John Kanyunyu aliyeko mji wa Sake, Mashariki ya Kongo hapa.

ZANZIBAR INAPIGA HATUA KUBWA KIAFYA



Duni:Afya Zanzibar imepiga hatua kubwa

duniLicha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya Zanzibar, imeelezwa kuwa katika miaka mitano iliyopita ya kutekeleza mpango mkakati namba mbili mabadiliko makubwa yamepatikana.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana, ni pamoja na Wizara ya Afya kuimarisha rasilimali watu ambapo idadi kubwa ya wafanyakazi wake wamepatiwa mafunzo ya ngazi na taaluma mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa saba wa Wizara ya Afya unaofanya mapitio ya utekelezaji wa mipango yake kwa mwaka unaomalizika huko katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Waziri wa wizara hiyo Juma Duni Haji, alisema kwa sasa, kuna wanafunzi 1,435 wanaopata mafunzo, ambapo 188 kati yao wako nje ya nchi.
Duni alieleza kuwa, huduma za afya zimeimarika Unguja na Pemba, sio tu kwa kuweka mamlaka na dhamana katika ngazi za wilaya, bali pia ugawaji wa rasilimali za watu, vifaaa na fedha.
Aidha, alisema ufanisi mkubwa umepatikana katika kuimarisha huduma za afya ya mtoto na mama kutokana na mikakati mizuri na utumiani bora wa raslimali adimu zinazopatikana.

CHANGAMOTOZINAZOIKABILI SUKZ


Changamoto za sasa zinazoikabili SUKZ


Viongozi wakuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.
(Imechukuliwa kutoka mtandao wa kijamii wa Facebook)
Mtazamo wangu ni tafauti na wengi walionitangulia, ila turudi katika malalamiko dhidi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKZ). Kwa jinsi hali ilivyo na mageuzi yaliyotegemewa baada ya kuundwa kwa SUKZ, tatizo kubwa lipo kutokana na kasi ndogo ya mabadiliko katika zile huduma muhimu za jamii. Na nafikiri wanasiasa watachukuwa dhima hii, kwani walipokuwa wanafanya kampeni zao, walionesha kama kwamba mabadiliko yatakuja siku moja.
Nina imani hata kama Chama cha Wananchi (CUF) kingelikuwa ndicho muundaji pekee wa serikali, basi kusingekuwa na tafauti kubwa katika kasi ya maendeleo kutokana na hali ya nchi ilivyo na ugumu wa msukumo wa gurudumu la maendeleo.
Ninaloliona mimi kwa sasa, changamoto kuu kwa SUKZ ni kusukuma kasi ya mabadiliko iendane na ahadi na matumaini waliyoyatoa wakati wa kuunda serikali.
Nafasi ngumu katika SUKZ haipo kwa CUF pekee, bali hata kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Ali Mohammed Shein kina changamoto nyingi kutoka kwa wale wahafidhina wasioutaka mfumo huu wa uundwaji wa serikali.
Ugumu kwa CCM Zanzibar ambao tumeona ukweli wao (walio wengi) hasa katika Baraza la Wawakilishi namna gani chachu ya mabadiliko inavyowasukuma katika uchangiaji wa hoja zao. Tatizo ni vitisho vya kufukuzwa au kusulubiwa kutoka kwa wachache ambao tangu mwanzoni walionekana kutokuwa tayari kuunda serikali ya mfano huu.
Sikubaliani na watu wanaposema CCM wengi hawakuutaka mfumo huu, ila kwanza na tuanze na tafsiri ya wengi ni kitu gani ikiwa asilimia 66 (kama sikosei) ya Wazanzibari, CCM na CUF, wote, waliunga mkono maridhiano na muundo wa serikali hii.
Ila nakubaliana na wingi wa walioukataa mfumo huu wakitokea CCM, bado uwingi wao huo (hata ikiwa wote ndio waliokataa) bado ni mdogo mbele ya umma ulioukubali mfumo huu.
Changamoto kubwa katika wapenda mabadiliko ndani ya CUF na CCM waliounda SUKZ kwa nguvu ya hoja na imani ya mabadiliko ni wahafidhina kutoka CCM na wale CUF waliochoka na kasi ndogo ya mabadiliko katika nchi.
Upande wa CCM wahafidhina kuona uwazi katika Baraza la Wawakilishi na umoja wa wawakilishi hao ni chungu isiyomezeka. Bado hawana njia madhubuti za kuwadhibiti wapenda mabadiliko katika CCM ambao ndio wengi walio na nafasi za chini. Nguvu za wengi hawa wapinga mageuzi kwenye CCM ni za midomo na kelele nyingi na sababu kuu ni kuchochea istifhamu za ndani ya SUKZ ili pavunjke turudi kwenye mizozano.
Kwa CUF wenye mbwembwe za kuukosoa mfumo wa SUKZ wao wana agenda yao moja pia, kuhakikisha historia ya CCM inaondoka visiwani. Hawa ndio wanaopingana na zile hekima za wakuu wa chama chao wanaohisi au wenye nia madhubuti ya kuwa na ushirikiano wa kweli na CCM wapenda mabadiliko na wenye muelekeo unaofanana.
Wengi wa kundi hili la CUF si wakaazi wa Zanzibar, na hufikira njia moja ya mambo haya kumaliza kadhia hizi ni kuingia katika mzozo wa kinguvu baina yao na wanaowaona kuwa wabishi wa mabadiliko hususan katika mfumo wa Muungano.
Ila wanasahau kwa nchi za kKafrika kushindana na dola hususan iliojaa vikosi visivyo na maadili hata za mafunzo juu yao wenyewe ni kukaribisha vifo vya watu ambavyo vinaweza kuepukwa. Hawatazami ushahidi uliopo katika nchi zilizokumbwa na majanga ya namna hii na mpaka hii leo hakuna hatua zilizochukuliwa na taasisi za nje zaidi ya kelele; na mwishowe nao wakasukumwa katika muundo wa serikali za umoja. Zimbabwe ni moja kati ya mfano mzuri. Kwa jinsi wanavyomchukia Rais Robert Mugabe na kumwachia atawale mpaka hii leo, ni vyema tukatathimini mafunzo yake.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar itafanikiwa, na itaendelea kuwepo na hatua baada ya hatua mabadiliko yatafuata. Kilichofanyika katika uchaguzi wa Bububu ni hekima za kweli baina ya vuguvugu la wanamageuzi ndani ya CUF na CCM. Kilichokusudiwa hasa hakijaonekana na kimetoweka, ni ushindi kwa vuguvugu la wanamageuzi kwa pande zote mbili.
Gurudumu linaendelea na mafunzo yapo na wapi pa kurekebiswa. Hii ni picha ya awali ya namna gani vyama vijiandee kwa uchaguzi mkuu wa 2015. Na kwa waheshimiwa wa pande zote wenye msukumo mmoja, wameziona changamoto hizi na wazifanyie kazi.
Tatizo kubwa la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kutoa matumaini makubwa yasiyoendana na hali ya ukweli wa nchi hususan kwa kuzingatia changamoto zilizopo baina ya vyama vinavyounda hii taasisi. Wakati umefika wa kuangalia mikakati mipya yenye kuweka vipaumbele kwa maendeleo ya wananchi hususan katika sekta ya afya, elimu, kilimo na ajira kwa wananchi. Mabadiliko yakianza huko, basi wepesi wa kusikilizwa na kufahamika ni rahisi.
Muungano ni suala la mabadiliko yanayotaka hekima itakayowajumuisha Wazanzibari wengi kuwa pamoja, katika kuunganisha nguvu. Ni sawa yapo baadhi ya mambo yatakayotakiwa kupatiwa muafaka ili kufikiwa lengo. Kama Muungano ulivyoundwa ukiwa na masuala machache mpaka sasa yamefika yaliyopo, basi na ufumbuzi wake unahitaji zaidi hatua hizo ziendane na wakati. Tutafika ikiwa busara na hekima zitatumika.

MATOKEO YA MAONI JUU YA KATIBA


Matokeo ya maoni juu ya katiba mpya zanzibar


Maoni leo asubuhi FUONI: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 54; na Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ili kuipa hadhi Zanzibar na Rais wake ni 74.
Maoni leo jioni KWARARA: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 54; na Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ya kuirejeshea Zanzibar nafasi yake kama mshiriki sawa ndani ya Muungano ni 71.

SMZ YAZUIA WATU WASISHUHUDIE KESI YA UAMSHO

SMZ yazuia watu wasishuhudie kesi ya Uamsho



Jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar, Vuga
Viongozi saba wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho walifikishwa katika Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar hivi leo, lakini chini ya ulinzi mkali wa karibuni vyombo vyote ya ulinzi na usalama, huku wananchi wakizuiwa kabisa kukaribia hata eneo la mahakama hiyo.
Askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiwemo wale wa Jeshi la Kujenga la Taifa (JKU), waliyazingira maeneo yote yanayokaribiana na jengo la Mahakama Kuu, huku wakiwazuia watu hata kukaribia jengo hilo. Watu wengi walioachangia maoni yao kupitia mitandao ya kijamii kuhusu namna kesi hii inavyoendeshwa, wamesema kwamba usiri, nguvu na vitisho vya hali ya juu vinavyooneshwa na SMZ katika muendelezo wa kesi hii, vinaashiria ukosefu wa uadilifu, woga na kutokujiamini kwa serikali mbele ya viongozi hao wa Uamsho iliowakamata.
“Hao (askari wa SMZ) hawana kazi za kufanya ndio maana wameambiwa nendeni mkakusanyike alau muonekane kama mpo. Na hiyo ni ushahidi kuwa hao Uamsho wana nguvu kuliko hao wanaoiendesha hiyo kesi….”, yalisomeka maoni ya mchangiaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Dula Said.
Mchangiaji mwengine aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Abbas Machano alisema kwamba binafsi alipita karibu na eneo la mahakama na akaona kwamba “mpaka njia ya kwendea Mnazi Mmoja imefungwa”, akiongeza kwamba hilo halikuwa  jambo la haki kwani “watu wanahitaji kupata taarifa.”
 Awaali mawakili wa viongozi hao walikuwa wamelalamikia kuwepo kwa jaji asiyeweza kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao  na hivyo wakawasilisha madai yao ya kubadilishiwa jaji mwenye uwezo wa kutoa maamuzi. Itakumbukwa kwamba tangu viongozi hao walipokamatwa kwa mara ya kwanza zaidi ya mwezi mmoja sasa, bado hawajapatiwa dhamana, licha ya dhamana zao kuwekwa wazi, lakini kwa masharti ambayo wengi wanaamini kwamba ni sawa na kulazimisha waendelee kubakia rumande wakati kesi yao ikiendelea kusikilizwa.
Kutokana na maombi ya mawakili hao, wamefanikiwa kuweza kubadilishiwa jaji ambae atakuwa na uwezo kwa kuitolea maamuzi kesi hiyo. Lakini katika tukio la leo, Jaji huyo aliweza tu kuwaita kwa majina yao na kisha kuahirisha  tena kedi hiyo hasi tarehe 6 Disemba 2012.