Friday, November 30, 2012

KIMATAIFA



Misri yapitisha rasimu ya katiba


MURSE
Bunge la Misri leo limepitisha mswada wa rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura na wananchi ili kuwa katiba kamili. Mwenyekiti wa bunge hilo Hossam el-Ghiriani ametangaza taarifa hizo mapema hii leo.
Bunge hilo linalotawaliwa na Chama cha Udugu wa Kiislamu ambalo linapingwa na Wakristo na Waliberali limepitisha vifungu 234 vya rasimu hiyo. Mswada huo utapelekwa kwa Rais Mohammed Mursi kwa ajili ya kutiwa saini na kisha kupigiwa kura wiki mbili zijazo. Upande wa upinzani nchini Misri umemtuhumu Rais Mursi na washirika wake kuwa wamepitia juu juu vifungu hivyo kwa lengo la kuupitisha muswada huo haraka ili upigiwe kura.
Kufuatia hatua hiyo, maandamano makubwa yamezuka yakipinga muswada huo. Katiba itakayopitishwa itachukua nafasi ya ile iliyoondolewa baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa taifa hilo Hosni Mubarak.

No comments:

Post a Comment