Friday, November 30, 2012

WAASI WA M23 BADO WAPO GOMA


Waasi wa M23 bado wapo Goma

Waasi wa M23 katika mji wa Goma, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi wa M23 katika mji wa Goma, Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa kutoka ndani ya maeneo ya mji wa Goma na Sake zinaonesha kwamba bado waasi wa kundi la M23 la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamo kwenye miji hiyo na wamefanya machache kuthibitisha kuondoka.
Umoja wa Mataifa umesema bado hakuna dalili za kuondoka kwa waasi kwenye mji wa Goma, zoezi ambalo ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa kumaliza mgogoro nchini humo. Naibu mMsemaji wa Umoja huo, Eduardo del Buey, amesema kuwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) vitaanza kuwaangalia waasi wa M23 waliouchukua mji wa Goma na sehemu kubwa ya jimbo la Kivu ya kaskazinilenye utajiri wa madini, kwa kutumia ndege zisizoendeshwa na rubani.
Taarifa zinasema kuwa kumekuwepo na misafara ya vikundi vidogovidogo vya M23 kuingia na kutoka katika eneo hilo lakini umoja wa mataifa hauna uhakika kama waasi hao wamepungua mjni Goma. Waasi wa M23 wamesema kuwa wataukabidhi mji huo kwa serikali hii leo au kesho.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle aliyetembelea eneo la Sake, anathibitisha kwamba bado wapiganaji wa M23 wanaendelea kushikilia ngome zao kwenye milima na viunga vya Sake, huku pia wakijihusisha na uporaji katika maeneo wanayoyakalia.

Sikiliza ripoti ya John Kanyunyu aliyeko mji wa Sake, Mashariki ya Kongo hapa.

No comments:

Post a Comment