Duni:Afya Zanzibar imepiga hatua kubwa
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana, ni pamoja na Wizara ya Afya kuimarisha rasilimali watu ambapo idadi kubwa ya wafanyakazi wake wamepatiwa mafunzo ya ngazi na taaluma mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa saba wa Wizara ya Afya unaofanya mapitio ya utekelezaji wa mipango yake kwa mwaka unaomalizika huko katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Waziri wa wizara hiyo Juma Duni Haji, alisema kwa sasa, kuna wanafunzi 1,435 wanaopata mafunzo, ambapo 188 kati yao wako nje ya nchi.
Duni alieleza kuwa, huduma za afya zimeimarika Unguja na Pemba, sio tu kwa kuweka mamlaka na dhamana katika ngazi za wilaya, bali pia ugawaji wa rasilimali za watu, vifaaa na fedha.
Aidha, alisema ufanisi mkubwa umepatikana katika kuimarisha huduma za afya ya mtoto na mama kutokana na mikakati mizuri na utumiani bora wa raslimali adimu zinazopatikana.
No comments:
Post a Comment