Wednesday, June 5, 2013

FAHAMU KUHUSU BOTI MPYA YA KAMPUNI LA S.S.B ILOSHUSHWA LEO ZANZIBAR

Boti mpya ya kisasa ya Azam Marine, Kilimanjaro IV ikiwa imeshushwa katika bahari ya Hindi eneo la Zanzibar  mchana wa leo tayari kuanza kazi kwa safari za Dar es Salaam na Zanzibar.

Mmiliki wa Makampuni ya S.S. Bakhresa, Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Maji Zanzibar (ZMA) na kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni yake, Jaffar Iddi 

Kilimanjaro IV kabla ya kushushwa kwenye Meli iliyoileta nchini

Inashushwa...

Inateremshwa majini

Azam Marine wamekarabati pia eneo la abiria kupumzika wakisubiri usafiri na mfumo mzima wa huduma hadi ofisi za kisasa

Ofisi mpya za Idara ya Uhamiaji Azam Marine

Ofisi mpya ya Polisi

Abiria wanastarehe sasa

Burudani kwenye Luninga kubwa wakati unangoja boti

Meneja Mkuu wa Azam Marine, Omar Mohamed Said kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kilimanjaro IV

Mzee Bakhresa alikuwa bize mpaka basi leo

Anatazama Meli inavyoshushwa

Mwonekano wa Nje unapoelekea kupanda boti za Azam Marine

Mzee Bakhresa na Jaffar Iddi nyuma

Mzee Bakhresa akifuatilia uteremshwaji wa Meli 

Mzee Bakhresa akitoa maelekezo

Namna hiyo, kila kitu kinakwenda sawa

Mzee Bakhresa

Mzee Bakhresa pembeni ya Abdulrazak, moja kati ya majembe ya Azam Marine(SANTE BIN ZUBERY )

Baaas, iwekeni hapo hapo na mtie nanga; Mzee Bakhresa akitoa maelekezo

MAMBO 12 YANAYOIFANYA BONGO MOVIE IDHARAULIKE


Pamoja na ukweli kwamba filamu za Tanzania zimefika katika hatua nzuri kwa sasa katika nyanja za uandishi, utayarishaji, usambazaji na mauzo ukilinganisha na miaka kama mitano iliyopita, bado kuna kasoro za hapa na pale. 


Kasoro ni nyingi kulingana na uchanga wa tasnia hiyo ukilinganisha na filamu za kimataifa lakini ni suala linaloweza kuvumilika kutokana na ukweli huo. 

Lakini kuna baadhi ya wadau wamekuja na sababu kadhaa za utani ambazo zinatambulisha filamu za Bongo nazo ni:

1. Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke barabara.

2. Matajiri majumba yao yana askari badala ya electric fence & gates.


3. Trailer inachukua dakika 40.


4. Part2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part1 ilikuwaje.


5. Mademu wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.


6. Wakifika hotelini imezoeleka ni juice inaagizwa au wine isiyofunguliwa.


7. Nusu saa mtu anatembea,anafanya mazoezi, anakimbizwa ananunua vitu.

8. Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.


9. Mtu yupo village, life gumu ana wave kichwani.


10. Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.


11. Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara.


12. Tajiri anakuja kumpenda maskini.