Monday, December 10, 2012

Tanzania bara yasherehekea siku ya uhuru


Tanzania bara itaadhimisha miaka 51 ya uhuru Jumapili (tarehe 9 Disemba) kwa kufanya gwaride mjini Dar es Salaam, gazeti la Tanzania la Daily News liliripoti.
Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Uhuru, mahali ambapo Tanzania ilishusha bendera ya Uingereza na kupandisha bendera ya Tanganyika huru tarehe 9 Disemba 1961.
Maadhimisho haya yatajumuisha ukaguzi wa rais Jakaya Kikwete wa gwaride la heshima, maonyesho ya ngoma za asili kutoka Dodoma, Ukerewe na Zanzibar, na maonyesho ya ngoma utakaofanywa na Rwanda National Ballet.
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Tanzania Minzengo Pinda na marais wastaafu Benjamin Mkapa na Ali Hussein Mwinyi watakuwepo katika sherehe hizo. Wakuu wa nchi sita za nje na mabalozi wa kidiplomasia wamealikwa pia kuhudhuria.

No comments:

Post a Comment