Amir Haji, mlezi wa Jumuiya
hiyo, alisema wamesikitishwa na taarifa zilizotolewa katika magazeti
mbali mbali ya hapa nchini likiwemo Tanzania Daima, Mtanzania, Zanzibar Leo na Uhuru yaliyomnukuu Sheikh Soraga huyo kuihusisha Uamsho kuhusika na tukio hilo.
“Uislamu unakataza kufanya
mambo maovu kwa kujidhuru mwenyewe au mtu mwengine aliye Muislamu na
asiyekuwa Muislamu”, alisema Amir Haji na kuongeza kuwa mara nyingi
Jumuiya hiyo imekuwa ikipakwa matope kuhusishwa na uovu kama huo ilhali
haina malengo hayo.
“Cha kusikitisha zaidi ni kiongozi Muislamu kusema maneno kama hayo
ya kutupaka matope. Shutuma hizi zimezidi mipaka na ndugu yetu Sheikh
Soraga amelipalia makaa. Kila siku tunapakwa matope. Lakini tunamuomba
kama hana la kusema basi anyamaze na kama ana ushahidi basi autoe katika
vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake“, alisema Amir Haji,
ambaye pia amemtaka Katibu huyo wa Mufti kuwaomba radhi Waislamu na
jumuiya hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa
Uamsho, Said Hamad, ameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kina wa
kubaini wahalifu waliotenda unyama wa kuwamwagia tindikali wasichana
wawili wa Kiingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa 18,
na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo kuendelea
hapa nchini.
Katibu huyo wa Uamsho aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano wa kina kwa jeshi la Polisi nchini ili
kufanikisha uchunguzi juu ya tukio hilo.
Uamsho yalalamikia watoto wa masheikh kutokuruhusiwa kuwaona baba zao
No comments:
Post a Comment