Umoja wa Mataifa waiunga mkono Palestina
Katika wakati ambapo mjadala kuhusu Muungano wa Tanzania umepamba moto visiwani Zanzibar, wachangiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii waliokuwa wakifuatilia moja kwa moja Mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, wamesema kwamba “sasa ni zamu ya Zanzibar”, wakimaanisha kwamba ni wakati wa Zanzibar kujitoa kwenye Muungano na kuchukua kiti chake Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, kura ya leo haimaanishi kwamba tayari Palestina imetambuliwa kuwa taifa na dola huru, ingawa ni muhimu sana kwa heshima yao na aibu kubwa kwa Israel na Marekani.
Balozi wa Marekani, Susane Rice, amelaumu hatua ya Hadhara Kuu kuipa hadhi ya uwanachama usio wa dola Palestina akisema kwamba haitabadilisha chochote kwenye maisha ya Wapalestina. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alisema kwamba msimamo wake unabakia ule ule wa dola mbili huru, ya Israel na Palestina, lakini lazima mataifa hayo yaishi kwa amani.
No comments:
Post a Comment