Wananchi Kinuni wataka Zanzibar yenye mamlaka kamili ikifuatiwa na Muungano wa Mkataba.
Katika kukusanya ya Maoni ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano, watu
wa shehia ya Kinuni, wilaya ya Magharibi Unguja, wamesema wanataka
kuiona Zanzibar ikiwa huru kwanza, halafu pawe na Muungano wa Mkataba
kati yake na Tanganyika. Jumla ya watu 135 walitoa msimamo huo mbele ya
wajumbe wa Tume ya Katiba juu ya katiba, huku
44 wakitaka mfumo wa sasa wa Muungano ubakie kama ulivyo.
No comments:
Post a Comment