Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa
Watu wasiojulikana wamemvamia askari polisi mmoja na kumjeruhi kwa
mapanga, mnamo majira ya saa 10:00 alasiri katika huko Mboriborini kando
kidogo ya mji wa Zanzibar. Imeripotiwa kwamba kundi hilo la watu
lilimvamia askari huyo anayejulikana kwa jina la Othman Juma na
kufanikiwa pia kuchukua pesa alizokuwa nazo ingawa haijajulikana ni
kiasi gani mpaka sasa. Hatua za kumpatia matibabu askari huyo
zinaendelea vizuri katika hospitali ya Al Rahma, Kilimani Unguja.
No comments:
Post a Comment