Bomu lililotegwa kando ya barabara katika eneo la Eastleigh jijini
Nairobi hapo Jumatano (tarehe 5 Disemba) lilimuua mtu mmoja na
kuwajeruhi wanane wengine, liliripoti shirika la habari la AFP.
Bomu hili "lilikuwa limekwa kwenye shimo ardhini", na lililipuwa wakati wa pilika nyingi Jumatano jioni wakati watu walipokuwa wakirudi nyumbani kutoka kazini, alisema mkuu wa polisi wa Nairobi, Moses Nyakwama.
"Mtu mmoja alikufa hospitalini na mwengine bado amelazwa," alisema Nyakwama akiongeza kwamba wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Shiurika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema hapo Alhamisi kwamba majeruhi aliyebakia hospitalini alikuwa katika hali mbaya sana.
Hakuna mtu aliyedai kubeba dhamana ya mashambulizi hayo.
Eneo hilo lenye kukaliwa kwa wingi wa watu wenye asili ya Somalia limeshuhuida kuongezeka kwa mashambulizi. Mwezi uliopita, kiasi cha watu watano waliuawa na zaidi ya 10 kujeruhiwa katika mashambulizi ya guruneti dhidi ya basi dogo. Mlipuko huo ulichochea ghasia za kikabila zilizojeruhi watu kadhaa.

No comments:
Post a Comment