Monday, December 10, 2012

Wasiwasi umeongezeka juu ya ubakaji katika makambi ya Wasomali


Vurugu dhidi ya wanawake wa Somali huongezea, hususani matukio ya ubakaji yanayohusisha watu wasio na makaazi nchini mwao (IDPs) huko Mogadishu na vitongoji vyake, wanaharakati wa haki za wanawake wamesema.
    Wanawake wa Somalia wanaoishi katika makambi ya watu wasio na makaazi nchini mwao huko Mogadishu na vitongoji vyake viko hasa katika hatari ya aina mbalimbali za vurugu. [Stringer/AFP]
  • Wanawake wa Somalia wanaoishi katika makambi ya watu wasio na makaazi nchini mwao huko Mogadishu na vitongoji vyake viko hasa katika hatari ya aina mbalimbali za vurugu. [Stringer/AFP]
Kwenye tukio la Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Utokemezaji wa Vurugu dhidi ya Wanawake tarehe 25 Novemba, wanaharakati wametoa wito wa jitihada kuongezwa kuzuia vurugu dhidi ya wanawake wa Somalia.
"Wanawake wa Somalia wanapatwa na aina mbalimbali za vurugu ambazo zinajumuisha ukeketaji, ndoa za kulazimishwa na ukatili wa majumbani, lakini ubakaji bado ni aina mbaya ya shambulio wanalokumbana nalo wanawake," alisema Zahra Mohamed wa Kituo cha Maendeleo cha Wanawake wa Somalia. "Tumesajili matukio ya ubakaji na majaribio ya ubakaji 126 kwa kipindi cha miezi minne pekee na uongezekaji huu mkubwa unatisha."
Alisema idadi kamili ya matukio ya ubakaji inaweza kuwa kubwa zaidi kwa sababu waathirika wengi hawaripoti uhalifu huu. "Kuna matukio mengi ambayo hayaripotiwi kwa sababu waathirika wanaona aibu kuzungumza kilichowatokea kwa sababu wanaogopa ubakaji unaweza kuwaletea aibu," aliiambia Sabahi. "Hii ni kwa sababu jamii ya Wasomali ni jamii isiyopenda mabadiliko na kuchukulia ubakaji kuwa jambo la kuaibisha ambalo linawajia mara kwa mara wanawake kwa kipindi kilichosalia cha maisha yao."
Kituo cha Maendeleo ya Wanawake cha Somalia kiliandaa semina ya siku mbili iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wa jamii ya Somalia huko Mogadishu iliyoanza tarehe 25 Novemba ili kutoa elimu ya haki za wanawake na kushughulikia aina za ukatili wa kimwili na kingono dhidi ya wanawake.

Wanawake katika kambi za watu wasio na makaazi nchini mwao (IDP) wanaathirika zaidi

"Uhalifu wa ubakaji na shambulio la kingono dhidi ya wanawake wanaoishi katika makambi ya Mogadishu umeongezeka," Mohamed alisema. "Hili linahitaji serikali na pande zote zinazohusika kuingilia kati kuondoa ukuaji sugu wa jambo hilo."
Waathirika wa ubakaji walio wengi wanaishi katika makambi ya IDP yaliyochakaa huko Mogadishu na vitongoji vyake ambavyo mara nyingi havina milango au miundo mingine ya kuzuia washambuliaji.
Kwa sababu hiyo, Samira Abdullahi, mwenyekiti wa Kituo cha Kuwalinda Waathirika wa Kubakwa Somalia, alisema waathirika wa kubakwa walio wengi ni wanawake wanaoishi makambini. "Asilimia tisini na tano ya matukio hayo yametokea katika makambi ya IDP wakati wabakaji walipovamia usiku na, kwa kushikiwa bunduki, walitishia kuwaua wanawake kama hawatakubaliana na matakwa yao," aliiambia Sabahi.
Abdullahi alisema makambi ya IDP huko Mogadishu hayana ulinzi -- ukiondoa kambi ya Badbaado inayosimamiwa na serikali ya Somalia na kambi ya Jazeera inayosimamiwa na Hilali Nyekundu ya Uturuki.
"Kulishughulikia jambo hili hakuwezi kufanyika kwa kutoa kauli mbiu na maneno matupu," alisema. "Tunaiomba serikali mpya kuchukua hatua za haraka za kuwalinda watu waliopoteza makazi."

Hadithi binafsi ya kubakwa katika kambi huko Mogadishu

"Wanawake wasiokuwa na makaazi nchini mwao hawajisikii salama kwa sababu hakuna anayeweza kuwalinda dhidi ya mashambulio ya vibaka na watu wanaotumia silaha," alisema Farhiya Ahmed, mama wa wasichana watatu mwenye umri wa miaka 43 katika kambi ya Kulmis huko Mogadishu katika wilaya ya Hodan.
"Wiki chache zilizopita, mmoja kati ya mabinti zangu ambaye ana umri wa miaka 17 alibakwa na watu wenye silaha," aliiambia Sabahi. "Msichana huyo alikwenda dukani karibu na kambi kununua mafuta ya kupikia na alipokuwa njiani, alivamiwa na wanaume watatu wenye silaha waliomvuta huku wakimuelekezea bunduki hadi kwenye jengo lililokuwa limejitenga na kumbaka huko."
"Msichana huyo alijaribu kulia kwa kutafuta msaada lakini watu hao wenye silaha walimpiga kwa kitako cha bunduki na kumpiga mateke," alisema. "Baada ya kumbaka, walitishia kumuua kama atamwambia mtu yeyote kuhusu kilichotokea."
Wakati wanawake wengi hawazungumzi kuhusu kubakwa kwa kuogopa kupewa adhabu na jamii, Ahmed alisema ni muhimu kushirikishana hadithi ya binti yake ili kuibua uelewa na kuzuia hili kutokea kwa wanawake wengine.
"Binti yangu bado ana hofu kwa sababu kundi hili la wabakaji limemuathiri kisaikolojia na kimwili," alisema.

Unajisi unawahatarisha wanawake

Malyun Sheikh Haider, mwanaharakati wa haki za wanawake na rais wa Kituo cha Tathmini na Maendeleo, alisema wanawake wa Somalia wako katika mazingira ya aina tofautitofauti ya unyanyasaji kama vile ukeketaji wa viungo vya uzazi vya kike, ndoa za kulazimishwa, kunyanyaswa kingono, kubakwa na ukatili wa majumbani.
Alisema unajisi unachangia kuongezeka kwa kiwango cha mashambulizi dhidi ya wanawake wasiokuwa na makaazi nchini mwao kwa sababu wahalifu wanajua wanaweza kufanya uhalifu bila kuadhibiwa. "Kimsingi, wahalifu wengi wanakimbia makosa yao na hii ni bahati mbaya sana," aliiambia Sabahi. "Wahalifu wanapaswa kuadhibiwa."
Haider alikubaliana na msimamo wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambaye ametoa onyo kali kwa jeshi la taifa la Somalia kuhakikisha ulinzi wa raia. "Mwanajeshi yeyote anayemuua mtu mwingine naye atahukumiwa kifo," Mohamud alisema Jumapili. "Mwanajeshi yeyote atakayembaka mtu atahukumiwa kifo."
"Wahalifu lazima washitakiwe kwa mujibu wa sheria kwa sababu wasichana wa Kisomali hawawezi kupoteza heshima yao wakati wambakaji wako huru na kuepuka mkono wa sheria," Haider alisema.

No comments:

Post a Comment