Sunday, December 9, 2012

Vikosi vya Somalia na AMISOM vyadhibiti Jowhar


Jesho la Taifa la Somalia (SNA), likisaidiwa na wanajeshi kutoka Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), vilichukua udhibiti wa Jowhar kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab mwishoni mwa wiki, Shirika la Habari la Taifa la Somalia liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 9 Disemba).
Vikosi hivyo vya washirika viliuteka uwanja wa ndege na maeneo ya karibu ya Burane na Mahaday kabla ya kuuteka mji, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Shabelle ya Kati. Bila ya kuendelea na vita, wanamgambo wa al-Shabaab waliukimbia mji na kuelekea kusikojulikana, shirika hilo la habari liliripoti.
SNA na AMISOM sasa wana udhibiti kamili wa Jowhar, alisema mkuu wa SNA Jenerali Abdikarin Yussuf Dego-badan, kwa mujibu wa Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Jowhar ni makazi ya pili kwa ukubwa katika Shabelle ya Kati kutekwa kutoka kwa kikundi cha wanamgambo wa al-Shabaab mwaka huu, kufuatia kukombolewa kwa Balad mwezi wa Juni.

No comments:

Post a Comment