Polisi nchini Kenya wameambia
BBC kuwa nambari ya kupiga wakati wa dharura 999 imeanza tena kutumika
baada ya miaka 15 ingawa watu wanapiga simu za utani.
Mwezi Julai mahakama iliamua kuwa polisi
werejeshe huduma hiyo mwishoni mwa mwezi Julai, lakini BBC ilipojaribu
kupiga simu hiyo haijibiwi kamwe.Wenyeji walilazimika kupiga nambari za simu ambazo zilikuwa ndefu sana kuweza kupata huduma za polisi wakati wa dhahrura.
Ilikuwa bora kwa wenyeji kwenda kwa kituo cha polisi kupata huduma walizohitaji au kuripoti kisa cha uhalifu kuliko kupiga simu kutaka kusaidiwa na polisi.
Mkuu wa polisi mjini Nairobi Benson Kibui aliambia BBC kuwa tangu nambari hii kuanza kutumika tena , watu wamekuwa wakipiga simu za utani wakijidai kutafuta hoteli.
Pia kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanajaribu kuona ikiwa inafanya kazi.
Mwanaharakati wa Kenya Okiyo Omtatah alikwenda mahakamani akitaka nambari hiyo kuanza kutumika tena .
No comments:
Post a Comment