Saturday, August 3, 2013

Rais mpya wa Iran ashika madaraka


Rais mteule wa Iran Hassan Rouhani anaapishwa katika sherehe mjini Tehran ambapo atapewa idhini ya kiongozi wa kidini nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei.
Hassan Rouhani
Rouhani ambaye alikuwa mpatanishi kwenye mazungumzo ya mradi wa nuklia wa Iran, alishinda uchaguzi wa urais nchini Iran katika duru ya kwanza.
Wakati wa kampeni zake rais huyo mteule aliahidi kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na alisema ataimarisha uhusiano kati ya taifa hilo na jamii ya kimataifa ambao uliharibika zaidi wakati wa utawala wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.

No comments:

Post a Comment